KILE kitabu kilichotokea kuwa gumzo kubwa kabla hakijatoka, cha 'jifunze Lingala' cha nguli wa miondoko ya muziki wa dansi hapa nchini, Tshimanga Kalala Assosaa 'Mtoto Mzuri', kimeingia sokoni leo, imefahamika.
Kwa mujibu wa Assosaa aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi, nyumbani kwake Mtaa Mindu, Upanga, jijini Dar es Salaam jana, kitabu hicho kinapatikana sehemu mbalimbali ya mitaa ya miji yote hapa nchini.Akizungumzia lengo la kutoa kitabu hicho chenye kurasa 56 na ambacho kimesheheni picha na baadhi ya vibao vya wakongwe wa Kongo (DRC), Assosaa alisema kuwa, amekusudia kuwasaidia watangazaji wanaopiga nyimbo za Bolingo bila kufahamu maana yake.
Aidha, Assosaa alieleza kuwa, kadhalika kitabu chake hicho kitakuwa msaada tosha kwa wanamuziki wa dansi wa Kitanzania wanaoimba vibao vya Bolingo pamoja na wale wanaofanya biashara kati ya hapa nchini na Kongo (DRC).
"Hili ni toleo la kwanza la kitabu hiki, ambako baadaye kikishasambaa na kuenea zaidi, nitaanza mkakati wa kutayarisha toleo la pili," alisema Assosaa, kati ya waimbaji mahiri hapa nchini, anayemiliki bendi yake binafsi iitwayo 'Bana Maquiz'.
UNYAYO KUINADI 'ENEMY' KWENYE TV LEO
NYOTA mpya wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’, Khamis Tambiko ‘Unyayo’ leo anatarajia kuanza kusambaza video ya kibao chake kipya, ‘Enemy’, kwenye vituo mbalimbali vya Televisheni kwa utambulisho.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Unyayo alisema kuwa, anaamini video ya kibao chake hicho itawashika mashabiki wengi wa Bongo Fleva kutokana na namna alivyokiandaa vema.
“Video hii naamini itakuwa funika bovu kutokana na kuinakishisha zaidi kwa kumshirikisha mkali wa sanaa ya uchekeshaji hapa nchini, aitwaye ‘Zimwi’,” alisema Unyayo.
Aidha, unyayo alieleza kuwa, baada ya kumaliza kuisambaza video ya kibao hicho kwenye vituo vya televisheni, ataanza kumalizia kuaandaa almbamu nzima itakayokamilika baadaye mwaka huu.
Khamis Tambiko 'Unyayo'
No comments:
Post a Comment