Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Muumin ambaye ni kati ya waimbaji nguli wanaotikisa vilivyo anga la muziki wa dansi hapa nchini, alisema amekusudia kuwadhihirishia mashabiki pamoja na wapenzi wa Twanga Pepeta kuwa, ametua katika bendi hiyo kikazi zaidi na kwamba hatokuwa na masihara jukwaani.
"Unajua, baadhi ya mashabiki na wapenzi wameshaanza kukubali kuwa, hapa Twanga mimi ndio mahali pangu hasa, ila tatizo limebaki kwa wengine kukosa imani na kuamini kuwa pengine huenda wakati wowote nikawapa kisogo, jambo ambalo binafsi silifikirii kabisa," alisema Muumin.
Aidha, muumin alieleza kuwa, hivi sasa yuko katika mchakato wa kuhakikisha anawapakulia mashabiki vibao motomoto kuanzia kwenye albamu ijayo ya Twanga Pepeta, inayotarajiwa kufyatuliwa hivi karibuni, ambako baadhi ya vibao hivyo tayari vimeshaanza kutumbuizwa kwenye kumbi huku vikiwa na sauti ya nguli huyo.
MAANDALIZI ONYESHO LA JAHAZI MODERN TAARAB, MANCHESTER MUSICA YAANZA KWA MBWEMBWE DAR...
MAANDALIZI ya lile onyesho maalum la pamoja kati ya mabingwa wa mipasho hapa nchini, Jahazi Modern Taarab 'Wana Nakshi Nakshi' na wakali wa miondoko ya muziki wa dansi, Manchester Musica 'Vijana wa Full Vipaji' yameanza kwa kishinndo jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wakurugenzi Wakuu wa makundi hayo, Jarome Mponda (Manchester) na Mzee Yussuf 'Mfalme' (Jahazi) walisema kuwa, wasanii wao wako katika mazoezi makali kujiandaa na onyesho hilo lililopangwa kurindima Mei 8, kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, jijini Dar es Salaam.
"Unajua, hii ni mara yetu ya kwanza sisi Wana Jahazi kufanya onyesho la pamoja na Manchester, kwahiyo hatuna budi kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha kuwa jamaa hawa hawatupigi bao kwa wao kupagawisha zaidi mashabiki zaidi yetu, kwenye ukumbi wetu wenyewe wa nyumbani," alisema Mfalme Yussuf.
Aidha, Mkurugenzi wa Manchester Musica, Jerome Mponda naye alieleza kuwa, hali iko hivyo pia hata kwao kwani nao wanafanya mazoezi ya kukata na shoka kambini kwao Mbagala Kilungule ili kujiweka sawa na onyesho hilo wakichelea kuzidiwa nguvu na wenzao hao wa Jahazi Modern.
Aidha, Mkurugenzi wa Manchester Musica, Jerome Mponda naye alieleza kuwa, hali iko hivyo pia hata kwao kwani nao wanafanya mazoezi ya kukata na shoka kambini kwao Mbagala Kilungule ili kujiweka sawa na onyesho hilo wakichelea kuzidiwa nguvu na wenzao hao wa Jahazi Modern.
MVUA KIDOGO TU, KIZAA ZAA JIJINI DAR...
MVUA ndogo iliyonyesha jana mchana jijini Dar es Salaam imeonekana kuleta madhara makubwa kwenye baadhi ya maeneo ya jiji hilo lenye wakazi wengi wakiwamo wanamuziki pamoja na wasanii wa fani mbalimbali za burudani hapa nchini.
Kati ya maeneo yaliyokumbwa na zahama la mafuriko yaliyotokana na mvua hizo ni Mtaa wa Soko Mjinga, Mtoni Mtongani, ambako familia kadhaa zilijikuta zikiacha shughuli zao kwa muda na kuanza kazi ya kuondoa maji yaliyovamia vyumbani mwao na kuleta uhalibifu mkubwa wa mali zao.
Mwandishi wetu aliyetembelea eneo la tukio alishuhudia namna hali halisi ilivyokuwa, ambako baadhi ya wakazi waliitupia lawama Halimashauri ya Manispaa kwa kupanga miundo mbinu mibovu ya barabara zenye mitaro yenye uwezo usiolingana na msongo wa maji pindi mvua zinapoandama.
"Unajua, hii yote visingetokea iwapo Manispaa ingerekebisha vema miundombinu yake, lakini wapi bwana, hawa jamaa sijui hela wanazipeleka wapi halafu wanatutengenezea barabara katika mtindo wa 'bora liende'," alisema Mohammed Mauji, mmoja wa wacharazaji gitaa kiongozi la Solo wa Jahazi Modern Taarab.
Mohammed Mauji
Moja ya nyumba iliyokumbwa na balaa la mafuriko jana huko Mtaa wa Soko Mjinga, Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam.
Maji yakiwa yameacha mkondo wa mfereji uliojengwa kando ya barabara na kusambaa kwenye makazi ya watu
Msichana akiokota baadhi ya viwalo vilivyokuwa vimesombwa na maji katika mafuriko hayo
Hapa ni mahali mfereji mmoja mdogo unapopokea maji kutoka katika mifereji mingine miwili mikubwa zaidi!!!
ZENA KUONEKANA TENA KWENYE 'POISON OF LOVE'
Na Abdallah Menssah
NYOTA wa kike wa tasnia ya filamu hapa nchini, Annan Shaaban ‘Zena’ hivi karibuni anatarajia kuanza kuonekana kwenye filamu mpya ya kwake mwenyewe, inayokwenda kwa jina la ‘Poison of Love’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Zena alisema kuwa, katika filamu hiyo iliyobeba ujumbe mzito juu ya athari za usiri na wasiwasi katika mapenzi, ameigiza kama Mhusika Mkuu akitumia jina la ‘Nina’.
“Baadhi ya nyota wengine niliowashirikisha katika filamu hiyo ambayo kiukweli naamini itakuwa moto wa kuoteambali kutokana na namna ninavyoiandaa ni Tazan, Tonny, Mzee Magali pamoja na Bi Mjata,” alisema Zena.
Aidha, Zena alieleza kuwa, filamu hiyo ambayo kwa sasa iko katika hatua ya uhariri kwenye Studio iitwayo ‘Yangu Vision’ iliyo chini ya Wilblod Antony, ambako baada ya baada wiki mbili itakuwa sokoni ikipatikana kwenye mikanda ya kawaida, VHS, VCD pamoja na DVD.
Kabla ya filamu hii, Zena alitikisa kwenye makundi kama ‘Hisia Connection’ na Jakaya Theatre alikoshiriki Tamthilia kadhaa ikiwamo ile ya ‘Kizunguzungu’ iliyokuwa ikirushwa kwenye runinga ya ITV, alishiriki kucheza filamu ya ‘Saturday Morning’.
Tanzania Daima Ijumaa, Aprili 8, 2011.
Annan Shaaban 'Zena'
No comments:
Post a Comment