Hii ni Pub bab' kubwa inayosifika kwa kuwa na huduma za kisasa kabisa, yenyewe iko maeneo ya Mbagala Kilungule jijini Dar es Salaam. Kati ya vinywaji vinywaji bomba vinavyopatikana kwenye Pub hii ni ile pombe ya ajab ambayo ukiiwasha kiberiti inawaka kama Petroli, iitwayo 'SAMBUKA'.
Mkung'utaji mahiri wa gitaa Kiongozi la Solo wa wakali wa miondoko ya dansi, Manchester Musica, Adam Hassan ameweka wazi kuwa, hana mpango wa kurejea katika bendi yake ya zamani ya Extra Bongo 'Next Level'.
Akizungumza katika ofisi za Blog hii, jijini Dar es Salaam jana, Adam alisema hana mpango wa kurejea Extra Bongo kutokana na kuwa, kipato anachokipata sasa akiwa na bendi ya Manchester Musica kinakidhi mahitaji yake yote muhimu.Aidha, Adam alisema kuwa, kinachomfanya aweke nadhiri ya kutorejea tena katika bendi hiyo inayoongozwa na Ally Choki ni mkakati wake wa kuhakikisha anafanya maisha kwa ajili ya pesa na si kujituma kwa manufaa ya 'kumnenepesha shetani wakati kiti anakonda'.
Hivi sasa Adam ndiye Kiongozi Mkuu wa bendi hiyo ya Manchester inayoundwa na wanamuziki wengi chipukizi lakini wenye umahiri wa hali ya juu katika kurindimisha burudani ya dansi hapa nchini.
Akizungumza katika ofisi za Blog hii jijini Dar es Salaam jana, Ammar alisema kuwa, kibao hicho amekirekodia katika Studio ya White Production iliyo chini ya mtayarishaji mashuhuri na maarufu hapa nchini, Stive White.
Aidha, Ammar aliyetumia jina la 'Simba Mtoto' katika kibao hicho, alieleza kuwa amejaribu kuchanganya ladha kwa kumshirikisha msanii mwingine wa miondoko hiyo ya Bongo Fleva, anayefahamika zaidi kwa jina la Mamba Mzee.
"Natarajia kuanza kukisambaza kibao hicho kwenye vituo mbalimbali vya radio hapa nchini mwanzoni mwa wiki ijayo kwa utambulisho rasmi kwa wapenzi pamoja na mashabiki wangu," alisema Ammar aliyeimba kibao 'Toto la Afrika' akiwa na Dar Modern.
Na Abdallah Menssah
MWIMBAJI mpya wa bendi ya muziki wa dansi, Joseph Venas ‘Wera Baba’ ameonekana kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki, katika maonyesho yao mbalimbali tangu alipojiunga rasmi na bendi hiyo majuma mawili yaliyopita.
Mwandishi wa habari hizi aliyehudhuria karibu maonyesho yote ya Manchester Musica, toka kujiunga kwa Wera Baba, alishuhudia namna mwimbaji huyo anavyoshangiliwa na mashabiki pamoja na wapenzi wa dansi kila anapopanda jukwaani kuimba.
Baadhi ya vibao vya Manchester Musica ambavyo, Wera Baba aliyejiunga na bendi hiyo akitokea Bwagamoyo Sound iliyokuwa chini ya Mwinjuma Muumin, anaviimba kwa ustadi mkubwa ni pamoja na ‘Pesa’, ‘Sina’, ‘Kijumbe wa Mtaa’, ‘Urithi wa Baba’, ‘Jackline’ na Haraka Haraka za Maisha’.
Katika mazungumzo yake na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Wera Baba alisema, amedhamiria kuwadhihirishia mashabiki wa Manchester Musica kuwa amejiunga na bendi hiyo ili kuiongezea makali na kuifanya iwe tishio zaidi.
“Hivi sasa niko katika mchakato wa hatua za mwanzo za maandalizi kibao changu cha kwanza ndani ya Manchester, kitakachoitwa ‘Dakika za Majeruhi’, ambacho nawahakikishia wapenzi pamoja na mashabiki kuwa kitakuwa funika bovu,” alisema Wera Baba.
Bambucha alisema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Kampuni nyingi zimekuwa zikihitaji kufanya naye muvi za Kibongo.
Huyu ni Mkurugenzi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi, Manchester Musica ambayo hivi sasa inakuja juu kwa kasi kwelikweli katika medani hiyo.
Huyu naye ni Chid Benz katika pozi la aina yake kama alivyonaswa hivi karibuni.
Huyu ni mtayarishaji maarufu wa filamu za Kibongo, Omary Mbega maarufu kama 'Director Ommy'
Chid Benz na Banana Zoro katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment